GENERAL NEWS,BURUDANI,MICHEZO,MASTAA BONGO,VIDEO
Binti wa miaka 11 nchini paraguay amepata mtoto aliyedai kubakwa na baba yake wa kambo, baada ya serikali ya nchi hiyo kumzuia asitoe mimba hiyo.
Madaktari wa nchi hiyo mji mkuu Asoncion wamesema binti na mtoto wanaendelea vizuri baada ya kujifungua kwa upasuaji.
Paraguay ni taifa linalo amini imani ya katoliki, ambapo mwanamke anaruhusiwa kutoa mimba pale tu afya yake inapokuwa hatarini.
Binti huyo alibakwa akiwa na miaka 10 na baba yake wa kambo akiwa na miaka 42 kwa sasa yupo rumande akisubiri kutajwa kwa kesi yake hiyo.Baba huyo amekanusha kufanya kitendo hicho.

No comments:
Post a Comment