Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts
Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts

4 August 2016

CHINA WAZINDUA BASI LA AINA YAKE

Basi hili sio la kawaida. mtu wangu wa heshima
Lina uwezo wa kubeba abiria 300 huku magari yakipita chini yake na hivyo kuepusha msongamano wa magari barabarari.
Sasa huu ni mfano wa kwanza ambao umefanyiwa majaribio kwenye mkoa wa Hebei nchini China.
Lina urefu wa mita 22 na upana wa mita 7.9.
Tayari serikali za Brazil, France, India na Indonesia zimeonyesha nia ya kutaka kununua basi hili ambalo limesanifiwa na wahandisi wa China.

23 July 2016

MOYES APATA KAZI TENA LIGI YA ENGLAND

GENERAL NEWS,BURUDANI,MICHEZO,MASTAA BONGO,VIDEO
David Moyes ameteuliwa na Sunderland kuwa meneja wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka minne. Meneja huyo wa zamani wa Everton na Manchester United, 53, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Sam Allardyce ambaye amepewa kazi ya kuwa meneja wa timu ya taifa ya England. “Nimechukua kazi katika klabu kubwa Uingereza, na kwa kuungwa mkono kwa kiasi kikubwa, nina hamu ya kufanya kazi tena katika Ligi Kuu ya England,” amesema Moyes. Meneja huyo amekuwa bila kazi tangu alipofukuzwa na Real Sociedad mwezi Novemba mwaka jana. Allardyce alithibitishwa kuwa meenja wa England siku ya Ijumaa.
Acha maoni yako mtu wangu wa muhimu

7 March 2016

MGUNDUZI WA BARUA PEPE(email) AFARIKI


Ray Tomlinson raia wa Marekani ambae ni mtu wa kwanza
kuvumbua utumaji wa barua pepe(email) amefariki dunia.
Tomlinson amefariki akiwa na umri wa miaka 74

Mgunduzi huyu aliibuka na wazo la kutuma ujumbe wa
kieletroniki kutoka mtu mmoja hadi mwingine kupitia
mitandao mbali mbali. Mwaka 1971.

Aliandika ujumbe wa kwanza wa barua pepe wakati akifanya
kazi Boston, kama Mhandisi wa Computer, pia alikua
mwanzilishi wa matumizi ya alama "at"(@)kuwa ndio alama
kuu ya utumaji wa barua pepe.
Wakati wa uhai wake Tomlinson alisema hawezi kukumbuka
barua pepe yake ya kwanza ilielezea nini.

24 January 2016

MAREKANI YAKUMBWA NA THELUJI KUBWA

Zaidi ya watu milioni 80katika  vitongoji 18wameathiriaka katikausafiri wa reli nandege kusitishwa huku watu 200000wakibaki bila ya umeme