7 March 2016

MGUNDUZI WA BARUA PEPE(email) AFARIKI


Ray Tomlinson raia wa Marekani ambae ni mtu wa kwanza
kuvumbua utumaji wa barua pepe(email) amefariki dunia.
Tomlinson amefariki akiwa na umri wa miaka 74

Mgunduzi huyu aliibuka na wazo la kutuma ujumbe wa
kieletroniki kutoka mtu mmoja hadi mwingine kupitia
mitandao mbali mbali. Mwaka 1971.

Aliandika ujumbe wa kwanza wa barua pepe wakati akifanya
kazi Boston, kama Mhandisi wa Computer, pia alikua
mwanzilishi wa matumizi ya alama "at"(@)kuwa ndio alama
kuu ya utumaji wa barua pepe.
Wakati wa uhai wake Tomlinson alisema hawezi kukumbuka
barua pepe yake ya kwanza ilielezea nini.

No comments: