25 October 2016

MAJINA 15 YA WANAOWANIA BALLON D OR 2016

GENERAL NEWS,BURUDANI,MICHEZO,MASTAA BONGO,VIDEO



Majina 15 ya wachezaji wanaowania Ballon d'Or 2016 yaliyotolewa na France Football mpaka sasa. Majina mengine 15 kufuatia.
Sergio Aguero (Manchester City), Pierre-Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund), Gareth Bale (Real Madrid), Gianluigi Buffon (Juventus), Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Kevin de Bruyne (Manchester City), Paulo Dybala (Juventus), Diego Godin (Atletico Madrid), Antoine Griezmann (Atletico Madrid), Gonzalo Higuain (Juventus), Zlatan Ibrahimovic (Manchester United), Andres Iniesta (Barcelona), Koke (Atletico Madrid), Toni Kroos (Real Madrid), Robert Levandowski (Bayern Munich). Wewe ungempa nani tuzo hiyoo kama mdau wa nguvu.

R.SANCHES ASHINDA TUZO NA KUMPIKU RASHFORD

GENERAL NEWS,BURUDANI,MICHEZO,MASTAA BONGO,VIDEO



Kiungo wa Bayern Munich Renato Sanches mchezaji wa timu ya taifa ureno ameshinda tuzo ya 'mchezaji wa dhahabu Ulaya' (European Golden boy award), akimpiku Marcus Rashford wa England na Manchester United. Renato, 19, ameshinda tuzo hiyo iliyowahi kuchukuliwa na Wayne Rooney, Raheem Sterling, Lionel Messi na Sergio Aguero. Ni tuzo anayopewa mchezaji bora zaidi Ulaya chini ya umri wa miaka 21. Sanches, ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Ureno, atakabidhiwa tuzo hiyo siku ya Jumatatu mjini Monte Carlo. Tuzo hiyo hupatikana kwa waandishi wa habari wa Ulaya kupiga kura, na ilianzishwa na gazeti la Tuttosport la Italia, na ndio ambalo limetangaza habari hizi kwenye ukurasa wake wa kwanza. Sanches amecheza mechi nane kwa Bayern msimu huu, baada ya kusajiliwa kwa pauni milioni 27.5. 

HANS WA YANGA NA KUFUKUZWA YANGA

GENERAL NEWS,BURUDANI,MICHEZO,MASTAA BONGO,VIDEO




ANAFUKUZWA KWASABABU ALIWAKATALIA WAKUBWA KUMRUDISHA ANKO NGASSA ALIPOVUNJA MKATABA WAKE NA FREE STATE STARS.
Namnukuu Hans 'siwezi kukubali Ngassa asajiliwe alafu tuwapoteze wachezaji watatu' akimaanisha (msuva,Juma Mahadhi na Kaseke) wangeweza kupoteza mwelekeo wao kama Ngassa angesajiwa na Yanga,kiufundi Ngassa alikuwa haitajiki kwenye timu kwasababu ya uwepo wa hao vijana watatu.baada ya kuwakatalia walipanga njia ya kumtoa Kocha Hans pale yanga pia zipo sababu kibao hata kwenye mechi ya simba na yanga kumweka msuva na chirwa nje na kumpanga Mahadhi pia yote ni shinikizo la viongozi.
Hans ni kocha ambae hakika Yanga na na mpira wa Tanzania kwa ujumla tutamkumbuka sana.

22 October 2016

ALIYO YAULIZA MBWANA SAMATA INSTAGRAM KUHUSU FARID

GENERAL NEWS,BURUDANI,MICHEZO,MASTAA BONGO,VIDEO

NI baada ya kuona kimya kuhusu swala la mchezaji wa AZAM FC Farid na ishu yake ya kwenda kufanya majaribio spain na kufanikiwa.

hivi ndivyo alivyo uliza samatta kwenye account yake ya instagram.

Tokeo la picha la faridi musa


samagoal77Asalam aleikhum? Niliposikia farid anaenda Spain kwa majaribio nilipata furaha sana kwa Kuwa niliamini kwa kipaji alichonacho asingeweshindwa majaribio ktk club ile aliyokuwa anakwenda na ndivyo ilivyokuwa furaha iliongezeka baada ya kusikia azam wamemruhusu kwenda kuanza Maisha ayo mapya ya soka ulaya,kwa nini niwe na furaha kwa sababu naamini maendeleo ya timu yetu ya taifa yatapiga hatua kwa haraka tukiwa na wachezaj wengi wanaocheza soka la kulipwa nje ya tanzania,(imani yangu)lakini kadri siku zinavyokwenda nimekuwa simsikii farid akiwa ktk club yake mpya na habari zilizopo ni Kuwa bado yuko tanzania,je ni kwa nini bado yupo tanzania wakati kila kitu kilishakwisha nani ana jibu la swali hili? Tafadhari?kuna nini nyuma ya pazia🤔