25 October 2016

R.SANCHES ASHINDA TUZO NA KUMPIKU RASHFORD

GENERAL NEWS,BURUDANI,MICHEZO,MASTAA BONGO,VIDEO



Kiungo wa Bayern Munich Renato Sanches mchezaji wa timu ya taifa ureno ameshinda tuzo ya 'mchezaji wa dhahabu Ulaya' (European Golden boy award), akimpiku Marcus Rashford wa England na Manchester United. Renato, 19, ameshinda tuzo hiyo iliyowahi kuchukuliwa na Wayne Rooney, Raheem Sterling, Lionel Messi na Sergio Aguero. Ni tuzo anayopewa mchezaji bora zaidi Ulaya chini ya umri wa miaka 21. Sanches, ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Ureno, atakabidhiwa tuzo hiyo siku ya Jumatatu mjini Monte Carlo. Tuzo hiyo hupatikana kwa waandishi wa habari wa Ulaya kupiga kura, na ilianzishwa na gazeti la Tuttosport la Italia, na ndio ambalo limetangaza habari hizi kwenye ukurasa wake wa kwanza. Sanches amecheza mechi nane kwa Bayern msimu huu, baada ya kusajiliwa kwa pauni milioni 27.5. 

No comments: