22 August 2015

IRAN YAZINDUA KOMBORA LAKE JIPYA

GENERAL NEWS,BURUDANI,MICHEZO,MASTAA BONGO,VIDEO

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo imezindua kombora jipya lenye usahihi wa juu na linalotumia fueli mango ambalo limepewa jina la Fateh 313.
Kombora hilo la teknolojia ya kisasa kabisa lina uwezo wa kulenga shabaha umbali wa kilomita 500 na limetengenezwa na wataalamu wa Taasisi ya Viwanda vya Anga katika Wizara ya Ulinzi ya Iran. Kombora hilo ambalo limeshafanyiwa majaribio kwa mafanikio limezinduliwa katika sherehe iliyohudhuriwa na Rais Hassan Rouhani kwa mnasaba wa Siku ya Kitaifa ya Viwanda vya Ulinzi.
Kombora la Fateh 313 ni kizazi cha kisasa kabisa cha makombora ambayo yanatumia fueli mango na yenye chombo erevu cha kulenga shabaha kilichotengenezwa hapa nchini.
Katika miaka ya hivi karibuni Iran imepata mafanikio makubwa katika sekta ya ulinzi ambapo sasa inajitosheleza katika uzalishaji wa zana na mifumo muhimu ya kijeshi. Iran imesisitiza mara kadhaa kuwa uwezo wake mkubwa wa kijeshi si tisho kwa nchi zingine bali sera zake za kijeshi zimejengeka katika msingi wa kujihami.

No comments: