7 August 2016

MAANDALIZI YATAKAYOFANIKISHA BIASHARA YAKO

MAANDALIZI YA BUSINESS PLAN ITAKAYOFANIKISHA BIASHARA YAKO
Maswali ambayo unatarajiwa uyajibu pale unapohitaji msaada wa kitaalamu katika kuandaa business plan yako.

Miongoni mwa maswali haya ni:
1. Aina ya biashara unayotaka kufanya/Unayofanya?
2. Je, biashara yako ni mpya au ipo tayari inaendelea?
3. Kama ni mpya kabisa umeshaiundia chombo cha
        kuiendesha, yaani umeshafanya usajili wa kampuni au jina la
        biashara?
4. Ni wapi unapokusudia kufungulia biashara yako?
5. Je, biashara yako unadhamiria kuiendesha/unaiendesha
        kwenye jengo la kupanga au ni jengo lako mwenyewe?
6. Je, mtaji wa biashara yako ni shilingi ngapi na kati ya hizo
        fedha taslimu ni kiasi gani na thamani ya vifaa ni kiasi gani?
7. Je, katika huo mtaji ni kiasi gani ni fedha zako mwenyewe na
        ni kiasi gani unatarajia kukipata kutoka kwa wawekezaji au
        kama mkopo?
8. Unadhamiria kuajiri wafanyakazi na kama ndivyo
       unadhamiria kuajri wangapi na kila mmoja unakusudia
       kumlipa shilingi ngapi kaa mshahara?
9.    Kama ni biashara inayoendelea, je, biashara yako
       imeandaliwa taarifa za fedha (mahesabu) za kila mwaka?
10. Je, unazo taarifa muhimu za soko unalokusudia kuingia na
       zile zinazowahusu washindani wako wa kibiashara?
11. Je, unao mpango mkakati wa utekelezaji? (implementation
       strategy)
12. Je, ni mambo gani yanakufanya uamini kwamba biashara
        yako itafanya vizuri kuliko wanavyofanya wapinzani wako
       kibiashara?
13. Ni vitu gani vinakupa imani kuwa bashara yako ina uimara au
       itakuwa na uimara? (strengths)
14. Ni vitu gani vinakusikitisha kwamba vinaweza kuwa ni udhaifu
       (weaknesses) katika biashara yako?
15. Je, kuna fursa (opportunities) unaziona abazo ukizitumia
       vizuri zitaongeza thamani ya biashara yako na kuifanya ikue
       haraka?
16. Je, ni mambo gani kwenye mazingira ya ndani na ya nje
       ambayo unahisi kuwa usipokuwa makini yanaweza kutishia
       uhai wa biashara yako (threats)
TAFAKARI CHUKUA HATUA

No comments: