Umoja wa Mataifa, umesema kuwa picha zilizonaswa na satelite zimethibitisha kuwa hekalu kuu katika mji wa kale wa Palmyra, Kaskazini mwa Syria, umeharibiwa.
Ripoti zaidi zinasema kuwa kumetokea mlipuko, katika hekalu ya Bel iliyoko mjini Palmyra, ambao unathibitiwa na wanamgambo wa Kiislamu wa Islamic State, IS.
Wataalamu wa kuchunguza picha za satelite wa Umoja wa Mataifa, Unosat, wamesema kuwa picha hizo zinaonyesha kuwa hekalu hiyo imeharibiwa kabisa.
Mkurugenzi wa Unosat, Einar Bjorgo ameiambia BBC kuwa, picha walizonasa zimeonyesha kuwa jengo kuu la hekalu hiyo imeharibiwa kabisa.
Amesema minara iliyokuwa karibu na jengo hilo pia zimeharibiwa.
Mtu mmoja anayeishi karibu na hekali hiyo, ameiambia BBC kuwa ukuta unaozunguka hekalu hiyo na lango kuu ndizo zimesalia.
No comments:
Post a Comment