27 August 2015

SABABU ZINAZOZIFANYA LIGI KUU BARA 2015/16 KUWA BORA ZAIDI NI HIZI

GENERAL NEWS,BURUDANI,MICHEZO,MASTAA BONGO,VIDEO



  1. Patrci Liewig na Stand United: Wengi wanajiuliza maswali kuhusiana na ujio wa Mfaransa huyo ambaye ni mara ya pili kufundisha Tanzania akianza msimu wa 2012/13 akifundisha Simba na sasa Stand United ambayo ni timu change inayoshiriki ligi ya Vodacom msimu wa pili na msimu uliopita ilinusurika kushuka baada yakumaliza nafasi ya 10 na kuambulia point 31 baada ya kucheza mechi 26
  2. Toto Africans : TOTO imerejea kwa mara nyingine kwenye Ligi ya Vodacom Tanzania kwa mara ya nne tangu ilipoanza kushiriki ligi hiyo na msimu huu inaonekana kujipinga zaidi kwa kusajili wachezaji wengi wenye uzoefu ikiwemo na kuboresha benchi lao la ufundi kwa kumleta kocha Mjerumani Martin Glerics
  3. Juma Kaseja :Kipa mkongwe Juma Kaseja amesajiliwa na klabu ya Mbeya City kwa mkataba wa miezi 6 akiwa kama mchezaji huru baada ya kujiondoa kwenye klabu ya Yanga mzunguko wa pili wa msimu uliopita lengo la kocha Juma Mwambusi ni kupata ubingwa msimu huu baada ya kufanya vizuri kwa kumaliza kwenye tano bora kwenye misimu miwili iliyopita tangu walipopanda kucheza Ligi ya Vodaco
  4. African Sports: 6.African Sports Kama ilivyo Mwadui, African Sports ni timu kongwe lakini ilishuka daraja kwa muda mrefu hadi msimu huu imerejea tena ikitokea Tanga ni moja ya timu inayotarajiwa kuongeza changamoto kwenye ushindani wa kupigania taji la Ligi ya Vodacom kutokana na usajili walio ufanya.
  5. Malalmiko kati ya timu na marefa: Je mwaka huu malalamiko dhidi ya Timu na Marefa yatapungua? Ni swala la Muda kabla hatujajionea hali halisI
  6. Hamisi Kiiza - Simba : baada ya kumkosa mshambuliaji wakimataifa raia wa Burundi Laudit Mavugo, uongozi wa Simba umeamua kumbebesha majukumu mchezaji Hamisi Kiiza wakimtaka afunge idadi kubwa ya mabao ili kuipa ubingwa timu hiyo ambayo imekuwa na mwenendo mbaya katika misimu mitatu iliyopita. Je atafanikiwa kufika viwango ivo?
  7. Mwadui FC : Hii nimara ya kwanza kwa Mwadui kushiriki Ligi ya Vodacom Tanzania Bara ikiwa chini ya kocha mzoefu Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ aliyewahi kuzifundisha timu mbalimbali nchini ikiwemo miamba ya soka Simba ambayo pia aliwahi kuichezea. Je Julio ataendelea kuipa timu hii mafanikio na hata kusumbua wakongwe?
  8. Allan Wanga : Baada ya klabu ya Yanga kuwapoka Azam kombe la Ligi ya Vodacom msimu uliopita kocha mpya aliyekuja kuifundisha timu hiyo ambao ni mabingwa wa Kombe la Kagame Stewart Hall aliamua kusaijili mshambuliaji atakaye saidiana na nahodha John Bocco ili kufunga mabao na chaguo lake la kwanza lilikuwa kwa Mkenya Allan Wanga aliyekuwa akikipiga El Merreikh ya Sudan. Je Wanga atafanikiwa kuipa Azam ubingwa?
  9. Yanga na Azam nani Bingwa? Je msimu huu nani atafanikiwa kutwaa tena ubingwa baina ya Yanga na Azam? Katika misimu mitatu iliyopita miamba hii ya soka imetwaa ubingwa kwa zamu? Je itakua ni wao au atapatikana bingwa mpya?
  10. Simba : Je huu utakua ni mwaka wa Simba kurudisha heshima? Simba wameonesha kuadilika toka wapate kocha mpya, Je mabadiliko hayo yatawasaidia kurudisha makali na heshima yao kwenye Ligi Kuu?


No comments: